Sunday, October 28, 2018

MARATHI YANAYO SUMBUA NA TIBA ZAKE

A . MATATIZO YA MZIO (ALLERGY) . MATATIZO mengi kuhusu maradhi katika mfumo wa kupumua hutokana na hisia kali sana dhidi ya baadhi ya vitu.Vitu hivi baadae humsababishia madhara maarufu kwa jina la Allergy. Mfano wa vitu
hivi ni: pamoja na baadhi ya vyakula; Kufisidika au kuharibika kwa maji (water pollution) ; Kufisidika au kuchafuka kwa hewa, kwa mfano vumbi (air
pollution) ; Mabadiliko ya hali ya anga au hewa na mabadiliko ya hali ya misimu; Kemikali, gesi, harufu mbaya au uvundo, moshi; Dawa za kumeza. Mafuta mazuri, hata harufu ya vipodozi au manukato; Na baadhi ya vitu vingine, ambavyo mtu havipendi na pengine humdhuru. Vumbi yaweza kusababisha mtu kupiga chafya,
baridi au moshi vinaweza kumfanya mtu kukohoa, kula baadhi ya vitu vinaweza kumfanya mtu kupata maradhi ya ngozi, kunusa au kupata harufu ya baadhi ya mafuta mazuri yanaweza kumfanya mtu aumwe na kichwa n.k. Hali zote hizi ni mifano ya mzio. Tiba kubwa ya mzio ni kuepukana na yale yote yanayosababisha mzio.
B. PUMU (ASTHMA) : Haya ni maradhi ambayo husibu mapafu na kumsababisha mgonjwa apate shida ya kupumua. SABABU: Yawezekana kusababishwa na vumbi, aina ya unga au vumbi litokanalo na maua, baadhi ya vyakula, mabadiliko ya hali ya hewa, wanyama kama paka na mbwa, aina ya bacteria, kuvuta sigara, pumu ya kurithi. n.k.
DALILI: (3) Mgonjwa hupata shida ya kupumua ndani
hewa safi ya oksijeni na kupumua nje hewa chafu ya kabondayoksaidi. (4) Wakati mwingine utamsikia mgonjwa akipumua anatoa sauti isiyokua ya kawaida (wheezing sound) hii ni kwa sababu ya wingi wa makohozi (mafua) yaliyosongamana ndani ya mapafu na kuzuia nafasi ya hewa. Mgonjwa hupata shida anapokua ndani ya chumba ambacho ndani yake hakuna hewa ya kutosha kwa sababu ya udogo au upungufu wa madirisha. Mgonjwa hupata nafuu baada ya kutoa na kutema makohozi na kukaa sehemu yenye hewa safi.(5) Kukohoa au kikohozi cha muda mrefu.
TIBA: Kanuni ya kwanza: Chukua bakuli yenye maji ya moto kisha udondoshee ndani yake matone kadhaa ya mafuta ya habatsoda. Kaa juu ya kiti halafu ujifunike shuka na usogeze bakuli lenye maji ya moto nahabat soda ili upate mvuke wake.
Tiba hii inaitwa Aromatherapy. Baada ya kufanya hivyo jipake mafuta ya habat soda mgongoni na kifuani halafu unywe mafuta ya habat soda matone matatu. Tumia kanuni hii kutwa mara mbili asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili.
Kanuni ya pili: Chukua asali nusu lita, juisi ya kitunguu saumu mili lita 200, unga wa habat soda vijiko vinne vikubwa, unga wa tangawizi vijiko viwili vikubwa, unga wa mdalasini kijiko kimoja kikubwa. Vyote changanya pamoja. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara tatu.
C. MAFUA (FLU NA COMMON COLD) . HAYA ni maradhi maarufu, ambayo huambukiza kwa urahisi kutoka kwa mgonjwa hadi kwa mtu mwingine.
TIBA: Chukua asali robo lita, unga wa tangawizi vijiko viwili vikubwa, unga wa mdalasini kijiko kimoja
kikubwa na unga wa habasoda vijiko viwili vikubwa. Changanya zote pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara tatu.
D. MATATIZO YA MASIKIO: Bila shaka viungo au mishipa ya masikio, pua na koo yameungana na yana uhusiano wa karibu. Kwa hivyo kiungo kimoja kikiathirika yawezekana viungo vingine kuathirika, ikiwa vishambulizi vya bacteria vitasambaa hadi sehemu nyingine. Sikio ni kiungo maalum katika viungo vya hisia ambayo kazi yake ni kusikia.

IJUE MINYOO NA TIBA KIASILI

Minyoo ni wadudu hatari ambao huingia tumboni mwa binadamu na kusababisha matatizo kadhaa ya kiafya. Ukubwa wa minyoo tumboni hutofautiana, kuna minyoo yenye urefu wa kuanzia inchi sita hadi inchi 26, ikitegemea imekaa kwa muda gani tumboni.
Kwa kawaida minyoo huingia tumboni kwa njia kuu mbili, ingawa zipo njia nyingine. Minyoo huingia tumboni kwa kula chakula kisicho salama au kwa njia ya ngozi, hasa kwa watu wanaopenda kutembea na kucheza bila viatu miguuni.
Watoto ndiyo wanao ambukizwa zaidi minyoo kwa njia ya ngozi kutokana na tabia yao ya kupenda kucheza bila viatu, tena wakiwa sehemu zisizo safi. Vile vile mtu anaweza kupata minyoo kwa kunywa maji yasiyo salama au kwa kuumwa na mbu, inzi na hata kwa njia ya kujamiana bila kinga.
Dalili za mtu mwenye minyoo ni pamoja na mtu kuwa na utapiamlo, kuonekana dhaifu na ngozi kupauka, kusumbuliwa na tumbo, kula sana na kusikia njaa muda mfupi baada ya kumaliza kula. Pia mtu mwenye minyoo huwa mwenye hasira kila mara.
TIBA YA NYANYA
Pamoja na tiba mbadala nyingine unazoweza kuzijua, nyanya imepewa nafasi ya kwanza katika kutibu tatizo hili kwa mafanikio makubwa na bila kuleta madhara kwa mtumiaji baada ya kumaliza tiba.
JINSI YA KUTUMIA NYANYA KAMA TIBA
Tayarisha nyanya mbili za ukubwa wa kawaida kwa kuziosha vizuri (inashauriwa uzioshe kwa maji ya moto ili kuua vijidudu, ikiwemo minyoo), zikatekate
Kisha changanya na chumvi pamoja na unga kiasi wa pilipili manga.
Kula mchanganyiko huo wa nyanya, chumvi kidogo na pilipili manga asubuhi kabla ya kunywa chai au kitu chochote. Fanya zoezi hilo mara moja kwa siku, kwa muda wa siku 15 au wiki mbili. Kwa kula nyanya hizo, minyoo wote waliyomo mwilini mwako wataondoka na kuacha tumbo lako safi.
Tiba hii inaweza pia kutumiwa na watoto, lakini kwa watoto wenye umri wa KUANZIA MIAKA MITATU TU na kuendelea, haishauriwi kutumiwa na watoto wadogo chini ya umri huo